Home Audio Washitakiwa Watatu wa TRA Wanaohusika na Utoroshaji Makontena Wapewa Dhamana…….Yupo Masamaki na...

Washitakiwa Watatu wa TRA Wanaohusika na Utoroshaji Makontena Wapewa Dhamana…….Yupo Masamaki na Wenzake Wawili

Mahakama kuu ya Tanzania imeridhia dhamana kwa washitakiwa watatu wa
mamlaka ya mapato Tanzania TRA wanaokabiliwa na mashitaka ya kutoa
makontena 329 bandarini bila kulipiwa kodi na kuisababishia serikali
hasara ya shilingi bilioni 12.7.

Maamuzi hayo ya mahakama kuu ya Tanzania yametokana na ombi
lililowakilishwa mahakamani hapo na washtakiwa watatu wakiongozwa
aliyekuwa Kamishina wa Forodha wa TRA Bw Tiagi Masamaki.

Jaji wa mahakama hiyo Bi Wilfrida Koroso, alisema dhamana kwa
washitakiwa hao watatu iko wazi kama watatimiza masharti sita yakiwemo
ya kulipa hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja huku pia wakitakiwa
kuwasilisha hati zao za kusafiri na kutakiwa kuwa na wadhamini
watakaokuwa na uwezo wa kusaini hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.

Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa Naibu
Kamishna wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki (Kulia)
akiwa na wenzake aliyekuwa Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,
Habibu Mponezya na Bulton Mponezya wakiwa katika Mahakama Kuu Tanzania
jijini Dar es Salaam jana wakisomewa shtaka linalowakikabili  la makosa
ya jinai na uhujumu uchumi.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI