Home Audio Faiza: Ushindi wa Sugu Hauna Faida Kwangu

Faiza: Ushindi wa Sugu Hauna Faida Kwangu

Lady Gaga wa Bongo, Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amefungukia ushindi wa mzazi mwenzake huyo na kudai kuwa haumsaidii chochote.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Akizungumza juzi na Ijumaa, Faiza alisema alivyosikia ushindi wa Sugu wala hakufurahi kwani alimchukulia kama mtu mwingine tu aliyeshinda.
“Mimi kwa kweli ushindi wa Sugu naona kama wa mtu mwingine, haunihusu wala kunisaidia chochote mimi na mwanangu. Yeye ana maisha yake na sisi tuna maisha yetu hivyo nikisema eti nimefurahi yeye kushinda nitakuwa nawadanganya,” alisema Faiza. 

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI