Home Audio Askari polisi afutwa kazi baada ya video kuonesha akipokea rushwa!

Askari polisi afutwa kazi baada ya video kuonesha akipokea rushwa!

JESHI
la Polisi mkoani Tanga limemfukuza kazi askari wa kikosi cha usalama
barabarani aliyetambulika kwa namba F. 785 CPL Anthony Temu (46) wa
kituo cha Polisi Kabuku kwa kosa la kufedhehesha jeshi hilo.

Akitoa
taarifa kwa vyombo ya habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa
Tanga, Zuberi Mwombeji amesema askari huyo amefukuzwa baada ya
kuthibitishwa kwa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
ikimuonyesha akiomba na kupokea rushwa wakati akitekeleza majukumu yake. 

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI